MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA AWATAKA WATANZANIA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VINADHIBITI MADAWA YA KULEVYA
Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Mohamed
Gharib Bilal amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyo
shughulikia udhibiti wa dawa za kulevya ili wausika wachukuliwe sheria.
Dr Bilal ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mbio za
mwenge wa uhuru zilizozinduliwa leo Mkoani Kagera .Aidha amesema kuwa licha ya
juhudi zinazofanywa bado tatizo la dawa za kulevya ni kubwa na kuwataka
wananchi kuwataja waagizaji na wasambazaji wa dawa hizo ili wachukuliwe hatua.
Dr.Bilal amewataka
wananchi kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea Rushwa vinavyochangia
kuwanyima haki baadhi ya watu na kujiepusha na maambukizi mapya ya Virusi vya
Ukimwi.
Kuhusu mchakato wa katiba mpya Dr.Bilal amewataka wananchi
kujitokeza kuipigia kura rasimu ya katiba mara Bunge maalumu la katiba litakapo
kamilisha kazi ya kuijadili.
Kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu ni “katiba ni Sheria
kuu ya Nchi jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba bora”.
Post a Comment