WANAFUNZI WANALAZIMIKA KULALA CHINI HUKO MTWARA
Wanafunzi 68 kati
ya 556 wa shule ya sekondari ya wasichana ya Bweni katika manispaa ya Mtwara Mikindani,
wanalazimika kulala chini kutokana na upungufu wa vitanda.
Shule hiyo ya
kidato cha kwanza hadi cha sita na ambayo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma,pia
haina uzio,jambo ambalo wananchi hupita eneo la shule hata nyakati za usiku.
Kaimu Mkurugenzi
wa Manispaa ya Mtwara Mikindani,Ernest Mwogi, ameyasema hayo alipokuwa akisoma
taarifa ya shule hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vitanda 32 vilivyotolewa na
Benki ya Posta tawi la Mtwara.
Mwongi amesema
kuwa hivi sasa shule ina vitanda 210 wakati mahitaji halisi ni vitanda 278.
Shule ya Sekondari
ya wasichana ya Mtwara, ilianzishwa mwaka 1956 wakati ikiwa na darasa la tano
hadi la sita na na mwaka 1962 shule hiyo ilianza kudahili wanafunzi wa
sekondari.
Post a Comment