VIFO VYA WATOTO KUTOKANA NA UGONJWA WA UKIMWI NI TISHIO NCHINI TANZANIA
Hatari ya kuongezeka kwa vifo vya watoto
vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi na maradhi nyemelezi,inatishia taifa la
Tanzania.
Hali hiyo
inatokana na kuwapo idadi ndogo ya watoto wanaopata huduma na tiba ya ugonjwa
huo kuwa chini ya asilimia 20 nchini humo.
Takwimu za shirika la Afya Duniani
(WHO) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa Tanzania ina watoto 230,000 wanaoishi na
VVU na kati yao ni asilimia 26 pekee wanapata matibabu huku asilimia 74 ikikosa
huduma hiyo.
Shirika la huduma za kichungaji
kwa watoto wanaoishi na VVU mkoani Pwani na Dar es Salaam chini ya Kanisa
Katoloki Jimbo Kuu la Dar es Salaam (Pasada), kwa kushirikiana na Shirika la
kimataifa la kuhudumia watoto Duniani (Unicef) wameanzisha mradi wa kupungunguza
hatari hiyo.
Mkurugenzi wa ushauri na Utetezi
wa Pasada na Meneja Mradi huo Jovina Tesha aliwaambia waandishi wa Habari hivi
karibuni jijini Dar es Salaam mara baada ya Unicef kutembelea mradi huo wa miaka miwili kuwa malengo makuu ni kupunguza magonjwa na vifo
kwa watoto wenye VVU.
Amesema kwa sasa wanatengeneza
walimu watoto 120 kupitia klabu zetu 20 zilizopo jijini Dar es Salaam, nao
watatoa elimu kwa watoto wenzao katika klabu na nyumba kwa nyumba na wakishawabaini,
wanaohitaji tiba wataanza na wengine wataendelea kupewa huduma nyingine.
Mradi huo ulibuniwa Novemba
mwaka jana na umeanza rasmi Januari mwaka huu.
Post a Comment