MTANGAZAJI

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO NJIRO KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA AFYA JIJINI ARUSHA

Zaidi ya watu mia tano jijini Arusha wanatarajia kupatiwa huduma ya utafiti na uchunguzi wa afya juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti,kisukari,na shinikizo la damu ikiwa ni katika kuhakiki afya kwa jamii na kupata huduma mapema .

Akizungumza mapema leo asubuhi Mkurugenzi wa Idara ya afya na kiasi wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Njiro ambaye pia ni daktari katika hospitali ya Lutherani Medical Center ya jijini Arusha Dr Peter Mabula ameiambia morning star redio kuwa huduma hiyo inatarajiwa kufanyika mapema april 6 mwaka huu katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato njiro.


Taarifa zinasema kuwa huduma hiyo itafanyika kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Arusha Idara ya afya na kiasi ya kanisa la waadventista wasabato, Chama cha madaktari wa wanawake Tanzania MEWATA Kanda ya kaskazini, pamoja na madaktari kutoka hospitali ya Lutheran medical centre, Lengo kuu likiwa ni kufanya huduma kwa vitendo ili kusaidia jamii kutambua na kuchukua hatua madhubuti za kimatibabu kabla ya kuzidiwa .


Hata hivyo wito umetolewa kwa wakazi wote wa jijini humo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kupatiwa vipimo na ushauri bure kuhusiana na afya zao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.