IDADI YA WALIOKUFA AJALI YA BASI LA LUHUYE YAONGEZEKA
Idadi ya
abiria waliokufa kutokana na ajali ya basi la Kampuni ya Luhuye katika Wilaya
ya Busega, mkoani Simiyu juzi imeongezeka kutoka 12 hadi 17.
Baadhi ya marehemu, akiwamo Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wa Sabato Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wametambuliwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo, alisema wawili kati yao, walifariki juzi jioni wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando.
Hata hivyo, Kamanda Mkumbo alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mmiliki wa basi hilo, Masalu Jackson (37)mkazi wa eneo la Majengo mapya, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, kwa ajili ya upelelezi wa kipolisi.
Aliwataja maiti waliotambuliwa kuwa ni Mchungaji huyo wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Thomas Mwita (40), naAfisa Elimu wa Shule Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga, Wangwe Maurice ( 30), ambao walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu.
Aliwataja
wengine, ambao pia walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Magu kuwa ni Mahemba Chacha (42), mkazi wa Wilaya ya Serengeti,
mkoani Mara, Rahma Kibera (32) mkazi wa Bugalika, jijini Mwanza,
Alex Masatu (42).
Ingawa hakutaja majina, Kamanda Mkumbo alisema majeruhi tisa waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Magu wametambuliwa na kwamba, wawili kati yao, hali zao ni mbaya.
Aliwataja wengine waliokufa jana wakati wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kuwa ni Sheta Msongoma (58), mkazi wa Nassa, Jimbo la Busega, mkoani Simiyu na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Baraka Alex.

Post a Comment