TAKUKURU YAELEZA SABABU ZA KUWEPO KWA RUSHWA
Imeelezwa kuwa mishahara midogo kwa wafanyakazi wa serikali
na taasisi zingine,ubutu wa sheria mbalimbali,watu wasio waadilifu kuchaguliwa
au kuteuliwa kushika nyadhifa za juu pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ni
miongoni mwa sababu zinazo sababisha kuwepo kwa rushwa.
Hayo yamebainishwa na afisa uchunguzi mkuu wa taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani iringa (TAKUKURU),Bw Akwilinusi Shiduki
wakati alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu wajibu wa vijana kupambana na adui rushwa.
Amesema vijana wanawajibu wa kutambua mchango wao katika
kupambana na rushwa kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara
ya 26,27 na 28 inavyosema,ambapo ameenda mbali zaidi kwa kusema sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa kifungu cha 39 kinatamka bayana kuwa kila mtu
mwenye taarifa ya vitendo vya rushwa anawajibu wa kutoa taarifa hiyo kwa
takukuru.
Shiduki amesema kuwa kuwepo kwa rushwa kunaweza kusababisha
kushuka kwa pato la taifa,kuvusha nyara za serikali,madini na madawa ya
kulevya,wananchi kukosa imani na serikali yao pamoja na kuwa na viongozi
wasiofaa katika ngazi mbalimbali.
Sanjari
na hayo afisa huyo amewataka vijana kuwa mfano wa kuigwa kwa kukataa na kukemea
rushwa kila inapojitokeza na kuto shawishi kutoa au kupokea rushwa ili kupata
au kutoa huduma kwa wanajamii au vijana wengine.
Post a Comment