SERIKALI YAWATAKA WAKULIMA KUTOLIPIZA KISASI
Serikali
wilayani Igunga mkoani Tabora imewataka wakulima wilayani humo kutolipiza
kisasi cha mauaji kwa wafugaji wa wilaya kishapu mkoa wa shinyanga.
Ushauri
huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Igunga Bwana Elibariki Kingu wakati
alipozungumza na wahanga wa tukio la mauaji ya wakulima watano wa wilaya ya
Igunga baada ya kushambuliwa kwa mikuki na mishale na wafugaji wenye asili ya
kitaturu kutoka wilaya ya kishapu mkoa wa shinyanga na kusababisha vifo vya
wakulima watano wa wilaya ya Igunga.
Aidha Bwana Kingu amewatupia lawama baadhi ya wataendaji wa kata na vijiji
kutofanya kazi zao kwa uadilifu na badala yake wamekuwa wakichukua rushwa
kutoka kwa wafugaji na hivyo kusababisha wafugaji hao kufanya wanavyotaka.
Machi 29
hadi 30 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika wilaya ya igunga kulitokea
mauaji ya wakulima watano na wengine kadhaa kujeruhiwa kwa wafugaji waliokuwa
wakidai maeneo ya mashamba ya wakulima ni mali yao , hali iliyopelekea mauaji hayo kutokea.
Post a Comment