MAHAKAMA KUU YAMTIA HATIANI MKAZI WA NYAMAMONGO KWA KUJARIBU KUUA
Penina Magabe alivyosasa baada ya kusikilizwa kesi ya kujaribu kuuwa |
Mahakama kuu mkoani Mara imemtia hatiani
mkazi wa kijiji cha Nyamongo Mwita
Mwikwabe kwa kujaribu kuumuua Penina Magabe mkazi wa kitongoji cha Nyichoka Wilayani
Serengeti.
Mwikwabe alitenda kosa hilo mapema septemba 8, 2008 majira ya saa moja usiku kwa
kumshambulia Penina kwa kumkata sehemu mbali za mwili wake kwa kutumia panga na
hatimaye kukimbia kijijini hapo akihamia Kijiji cha Nyamongo Wilayani Tarime.
Mwendesha mashitaka wakili wa Serikali Monica Hokororo na Valence Mayenga waliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa baada ya kutenda kosa hilo alihamisha familia yake kwa kutumia lori aina ya fuso kwenda Nyamongo wilayani humo hata hivyo septemba 9, 2008 alikamatawa na jeshi la polisi na kurudishwa Wilayani Serengeti.
Mwanasheria wa serikali Venance Myaenga amedai kuwa Mwikwabe alitenda kosa hilo kwa kuvunja kifungu cha sheria ya adhabu namba 211(A) sura ya 16 kama ilivyorekebishwa mwaka 2012.
Na Waitara Meng'anyi-Tarime
Post a Comment