MTANGAZAJI

KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWAIKOSESHA TANZANIA KWENYE ORODHA YA NCHI ZINAZOFANYA VYEMA KATIKA UTAWALA BORA

Imeelezwa kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi ni moja ya sababu ya Tanzania kutoweza kuwa kwenye orodha ya nchi zinazofanya vizuri kwenye maswala ya utawala bora kimataifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora nchini Tanzania ,Kapteni mstaafu Geogre Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano na wajumbe wa baraza la ushauri wa mkoa wa dodoma .


Bwana Mkuchika ameongeza kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vimeiporomosha Tanzania hadi kufikia nchi ya 102 kati ya nchi 176 kwa mwaka 2013,huku mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)pamoja na mauji ya vikongwe kwenye baadhi ya mikoa nchini yaimeifanya Tanzania kufanya vibaya kimataifa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.