MTANGAZAJI

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MLAMKE IRINGA WATOA MSAADA KWA WATOTO

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mlamke Manispaa ya Iringa wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki nne na elfu sitini kwa kituo cha kulelea watoto waishio kwenye mazingira magumu.

Walimu wa shule hiyo Lusungo Ndondole na Frolensina Mguhunde,wakizungumza na mwandishi wa habari hii wakati wa kukabidhi msaada huo hivi karibuni kwa kituo cha Felix Nikosia,kilichopo kijiji cha Image wilaya ya Kilolo,wamesema kazi ya mwalimu ni kuelimisha na kufundisha upendo hivyo wameomba kuwepo kwa harambee za kusaidia makundi maalumu.


Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo Ezekia Mbyopo na Kwini Meenga wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema watu wawe na tabia ya kutembelea vituo hivyo ili wajionee hali halisi na kufahamu kuwa watu wote ni walezi wa yatima.


Awali akipokea msaada huo wa viatu,mashuka,nguo,unga na mchele msimamizi mkuu wa kituo hicho Bi Fausta Chota amesema kituo hicho kinahudumia watoto zaidi ya 100.


Na Augustino Kiyombo

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.