MTANGAZAJI

JAMII YATAKIWA KUTUMIA MKAA WA UNAOTOKANA NA NYASI NA TAKATAKA

Jamii imetakiwa kupunguza ukataji wa miti kwa kuwa na njia mbadala ya kudumu ya kutengeneza mkaa unaotokana na nyasi na takataka zinazopatikana katika mazingira yao.

Hayo yamebainishwa na Victoria Kabigi ambaye ni Mkufunzi wa kikundi cha jumuiya ya wanawake wajasiliamali wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (teku) alipozungumza na mwandishi wa habari hii ilipotembelea kwenye banda la maonyesho la wanawake hao kwenye viwanja vya Uyui Manispaa ya Tabora wakati wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


Kabigi ameeleza kuwa wakinamama wajasiriamali wa teku wameanzisha mradi huo wa kutengeneza mkaa mbadala ya mkaa wa miti ili kupunguza ukataji wa miti ovyo ambao unasababisha uharibifu wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.


Mafunzo hayo yatawawezesha wanawake kuwa na uelewa wa kutengeneza mkaa huo unaotokana na nyasi na takataka za mijini na mashambani jambo ambalo litasaidia kupunguza migogoro ya ndoa katika familia kutokana na wanawake kutumia muda mfupi kutafuta maji na hivyo kufanya ndoa zao kuimarika, na kuhifadhi vyanzo hivyo vya maji mifugo itaweza kupata maji ya kutosha


Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu mkoani Tabora yamefanyika kwenye viwanja vya Uyui manispaa ya Tabora ambapo jumla ya vikundi 32 vya ujasiriamali vimeshiriki.


Na:Fred Angaya

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.