MKAKATI WA USAFI JIJINI ARUSHA
Wakazi wa
jiji la Arusha wameipongeza serikali na manispaa ya jiji hilo kwa kutekeleza
moja ya mikakati yake ya kulifanya jiji kuwa safi na lenye hadhi ya miji
ya kitalii hapa nchini .
Moja ya utekelezaji wa mikakati hiyo ni
kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwa wakiendea na biashara
katikati ya mji na pembezoni mwa
Barabara,kubomoa vibanda na nyumba zote ambazo hazina hadhi ya kuwepo katikati
ya mji ,huku lengo ni kuhakikisha
mpangilio bora wa nyumba zilizoko mjini.
Mpango huo
umetekelezwa kufuatia amri iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela
ya kuwaondoa wafanyabiashara hao maarufu
kama machinga wasifanye biashara zao katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria.
Kwa mujibu
wa tathmini iliyofanywa na mwandishi wa habari hii imeonyesha kuwa sheria na mpango huo
umetekelezwa kwa asilimia tisini na tano huku waliokuwa wanategemea biashara
hizo wakiwa hawana eneo maalum la kuendelezea shughuli zao za kila siku.
Post a Comment