AJALI YASABABISHA VIFO MWANZA
Watu
watatu wamefariki na wengine kujeruhiwa vibaya hadi kulazwa
Hospitalini,kufuatia ajali mbili za magari zilizotokea jana na leo katika
maeneo tofauto jijini Mwanza.
Leo,
majira ya asubuhi huko Misungwi Mkoani Mwanza, watu watatu wamefariki na
wengine ambao idadi yao haijafahamika wamejeruhiwa vibaya,kati yao wanne
wamelazwa hospitalini hali zao zikiwa mahututi.
Ofisa
Mwandamizi wa Makosa ya Jinai Mkoani Mwanza, aliyezungumza na Redio Morning
Star Fm leo mchana, amesema ajali hiyo imetokea wilayani Misungwi Mkoani
Mwanza.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza,Valentino Mlowola
kuzungumza kuhusu ajali hiyo hazikufanikiwa,kwa taarifa kuwa alikuwa katika vikao.
Hata
hivyo, habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zimesema,Kamanda Mlowola angetoa
taarifa za ajali hiyo,baadaye alasiri leo
Mpaka mwandishi wa habari hii anatuma taarifa hii waliokufa katika ajali
hiyo,walikuwa hawajatambuliwa; na Kamaanda wa Polisi Mwanza alitarajiwa kutaja
majina yao katika mkutano na wanahabari baadaye leo.
Wakati
huo huo, ajali iliyotokea jana majira ya mchana katika eneo la Buzuruga,Nyakato
jijini Mwanza ilisababisha watu kadhaa kupata majeraha na kutibiwa hospitalini.
Sababu za
kutokea ajali za mara kwa mara jijini Mwanza zimetajwa kuwa ni mwendo kasi na
uzembe wa madereva,hususan katika misongamano ya magari katika njia kuu za
lami,ambako madereva huenda mwendo kasi pasipokuzingatia sheria za barabarani.
Na:Conges Mramba
Na:Conges Mramba
Post a Comment