MEWATA KUFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI KWA WANAWAKE JIJINI MWANZA
Chama
cha Madaktari wanawake Tanzania(MEWATA)kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii na taasisi zingine,kitazindua Uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi,Machi
8 mwaka huu jijini Mwanza.
Taarifa
ya MEWATA iliyosainiwa na Mwenyekiti wake,Dk. Sarafina Mkuwa na kutolewa kwa
vyombo ya habari hii leo jijini Mwanza inasema , zoezi hilo la uchunguzi kwa akina mama wa Kanda ya Ziwa litafanyika katika
uwanja wa Nyamagana kwa siku mbili
kuanzia Machi 8 hadi 9 mwaka huu.
Vituo
vingine ambavyo zoezi hilo litafanywa ni Hospitali ya Nyamagana,Hospitali ya
Wilaya ya Misungwi,Kituo cha Afya cha Misasi,Kituo cha Afya cha Buzuruga na
Uwanja wa Shule ya Msingi Mirongo.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mama
Salma Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA).
Mama
Kikwete atakabidhi mashine 16 za
kuchunguza saratani ya Mlango wa kizazi aina ya sikrotherapi (Cryotherapy) kwa
waganga wakuu wa mikoa minne ya Mwanza, Mbeya,Iringa na Mara.
Haarifa
zinasema kuwa Tanzania inaongoza kwa
wagonjwa wa maradhi hayo Afrika
Mashariki wakati kila mwaka wanawake 6,200 hugundulika kuathiriwa na maradhi
haya,wakati kati yao wanawake 4,000 hufariki dunia kwa maradhi hayo
Hadi
sasa kuna vituo 130 hapa nchini vya
kuchunguza saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi katika mikoa 17.
Na:Conges Mramba-Mwanza
Post a Comment