MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YATOA TAHADHARI YA KUNYESHA MVUA KUBWA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza
uwezekano wa kunyesha mvua kubwa zinazoweza kuleta maafa katika baadhi ya mikoa
ya Ukanda wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa ya tahadhari ya TMA
iliyotolewa jana imeeleza kuwa mikoa
itakayoathirika na mvua hizo ni pamoja na Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es
Salaam, Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba mjini Zanzibar.
Taarifa
hiyo inasema mvua hizo zinategemewa kunyesha kati ya Machi 05 hadi 07 mwaka 2014 na zitakuwa ni mvua kubwa
inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, ikiwa ni kiwango cha wastani (65%).
Taarifa
imefafanua kuwa hali hiyo inatokana na kuimalika kwa mgandamizo mdogo wa hewa
mashariki mwa bahari ya Hindi sambamba na kusogea kwa haraka kwa mfumo wa mvua
za msimu hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo
husika.
Hata
hivyo Taarifa hiyo imefafanua kuwa mvua
zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha zinaashiria kuanza mapema kwa mvua za
masika katika baadhi ya maeneo ya pwani ya kaskazini ikiwemo Dar es Salaam,”
imesema taarifa hiyo
Post a Comment