MTANGAZAJI

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YAWATAHADHARISHA WANANCHI

Mamlaka ya hali hewa nchini Tanzania  imetahadharisha juu ya kuwepo na mvua kubwa katika maeneo ya mwambao wa bahari ya hindi.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo inasema kuwa mvua hizo zinazozidi milimita hamsini zitasababishwa na kimbunga kinachoitwa Helen.


Mamlaka hiyo imesema kuwa mvua hizo zilitarajiwa kuanza jana hadi kesho, na kuyataja maeneo yatakayo kumbwa kuwa ni pamoja Dar es salaam , Mtwara ,lindi,Tanga,unguja na pemba.


Maeneo mengine ni mikoa ya Singida,Dodoma, Ruvuma, Katavi Njombe, Mbeya, na Morogoro ambayo mamlaka hiyo imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari watumiaji wa bahari pamoja mamlaka zinazohusika na maafa kuchukua tahadhari


Mamlaka hiyo imefafanua kuwa uwezekano wa mvua hizo ni asilimia 80 na ni mwendelezo wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.