MTANGAZAJI

RAIS KIKWETE AMEWASILI LONDON

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini London Uingereza kwa ziara ya siku tatu ya kidola.

Rais kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa jumamosi kuelekea mjini London kwa ziara hiyo ambapo atakuwa mgeni rasmi wa serikali uingereza.


Katika zira hiyo rais kikwete ameambatana na mkewe Mama Salma Kikwete,na mawaziri kadhaa wakiwemo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe, Waziri wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dk Hussein Mwinyi ,na Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.


Wengine ni waziri wa nishati na madini professor Sospeter Muhongo, Waziri wa fedha Saada Mkuya, Waziri wa biashara na masoko wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Nassor Mazuruhi, Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simba Kalia na Naibu wa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba .

Baada ya ziara ya uingereza Rais kikwete anatarajiwa kwenda Brussels ubeligiji kuudhuria mkutano wa nne wa wakuu wa nchi za umoja wa ulaya na afrika uliopangwa kufanyika siku ya jumatano na alhamis wiki hii
Mkutano huo ambao mada yake kuu itakuwa ni umuhimu wa kuwekeza katika watu ustawi na Amani utahudhuriwa na wakuu wa nchi wanachama wa AU na wale wa afrika akiwemo Rais kikwete.


Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais kikwete kuudhuria mkutano huo tangu achaguliwe kuwa Rais mwishoni mwa mwaka 2005.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.