MTANGAZAJI

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MAGOMENI MWEMBECHAI KUTOA MISAADA KWA WAFUNGWA

Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni mwembe chai linatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni tano za kitanzania kwa ajili ya misaada ya kijamii na kiroho kwa wafungwa na maabusu wa magereza yaliyopo mkoani pwani.

Kiongozi wa huduma za magereza wa kanisa hilo Bi,Amina Kikula amesema kuwa misaada itakayo tolewa ni Televisheni 3, king’amuzi,sabuni,vitabu pamoja na dawa za meno ambayo imetokana na michango ya waumini wa kanisa hilo.


Magereza yatakayo nufaika na misaada hiyo itakayotolewa machi 15 mwaka huu ni kigongoni Bagamoyo,Mkuza Kibaha na Bwawani.


Kanisa la Waadventista Wasabato magomeni Mwembe chai limekuwa likitoa misaada ya kijamii na kiroho kwa wafungwa na mabusu tangu mwaka 1999 katika magereza 11 yaliyopo Dar es salaam,Dodoma na Pwani.


Na:Ester Malekana

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.