MTANGAZAJI

NYUMBA TATU ZATEKETEZWA HUKO TARIME TANZANIA

Watu wasiofahamika wameteketeza nyumba tatu za nyasi mali ya Ghati Mwita katika kijiji cha Tagota kata ya Turwa wilayani Tarime.

Tukio hilo lilitokea mapema juma hili ambapo mali yote iliyokuwepo ndani ya nyumba hizo iliteketea kwa moto.Huku chanzo kikitajwa kuwa ni kulipizwa kisasi baada ya Bi Ghati Mwita kutuhumiwa kutekeleza mauaji kijijini hapo na kisha kutoroka.

Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.