WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
Marehemu Kamanda Liberatus Barlow enzi za uhai wake,picha kwa hisani ya kingjofa.blogspot.com |
Wakili wa Serikali Mkuu Mfawidhi Mkoani Mwanza,Timon Vitalis, amewaambia waandishi wa habari jijini Mwanza kwamba kesi hiyo ya tuhuma za mauaji nambari 30 ya mwaka 2012 ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mwanza.
Bwana Timon amesema, wanalipitia faili la kesi hiyo ili kujiridhisha kama upande wa mashitaka utakuwa na hoja katika shauri hilo litakapofunguliwa mahakama kuu baadaye mwaka huu.
Wanaosota rumande hadi sasa kwa tuhuma za kumuua Kamanda Barlow ni Muganyizi Peter,Chacha Mwita,Magige Marwa,Buganzi Luseta, Bhoke Mwita na watuhumiwa wenzao wawili ambao ni wakazi wa Mwanza na Dar es salaam.
Marehemu Barlow aliuwawa kwa kupigwa risasi tarehe 13 october 2012 majira ya saa saba usiku katika eneo la kitangiri jijini mwanza na genge la majambazi alipokuwa akitokea katika kikao cha harusi ya ndugu yake kilichokuwa kimefanyika katika hotel ya florida jijini Mwanza.
Post a Comment