MTANGAZAJI

MZAZI MWENYE MTOTO MTORO SHULENI HUKO URAMBO KUPATA ADHABU

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Urambo mkoani Tabora limepitisha sheria ndogo ya adhabu kwa mzazi ambaye mtoto wake atapatikana na kosa la utoro shuleni.

Adhabu iliyopitishwa na baraza hilo ni faini ya shilingi laki tatu au kifungo cha miezi kumi na miwili jela au vyote kwa pamoja


Akizungumzia sheria hiyo ndogo ya adhabu iliyowekwa,Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya urambo mhandisi Richard Ruyango amesema sheria hiyo imewekwa ili kudhibiti vitendo vya utoro uliokithiri kwenye shule za halmashauri ya wilaya hiyo na itasaidia wazazi kuelewa wajibu wao kwa watoto kwa kuwahimiza kuhudhuria shuleni


Wakizungumza na Fred Angaya wa  Morning Star Radio baadhi ya wazazi wilayani humo Dominic Mtasha na Theofil Msafiri wameomba kupunguzwa kwa adhabu hiyo iliyotungwa na kupitishwa na baraza la m
madiwani kuwa ni kubwa mno.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.