MTANGAZAJI

UTUMIKISHWAJI WA WATOTO MKOANI TABORA

Mtoto akipanga majani ya tumbaku (Picha kwa hisani ya kapipij.blogspot.com)

Halmashauri za wilaya mkoani tabora zimeweza kuondoa  watoto 4,546
wenye umri chini ya miaka 18 katika mazingira hatarishi na
utumikishwaji kwenye mashamba ya tumbaku.


Wakiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kwenye kikao cha
kamati ya  ushauri ya mkoa Wakurugenzi wa halmashauri wameeleza
kuwa  halmashauri ya wilaya ya Urambo na Kaliua zimewaondoa watoto
726 kati yao wa kiume ni 322 na wa kike wakiwa 404.


Nayo halmashauri ya wilaya ya Sikonge imeweza kuwaondoa jumla ya
watoto 1,274 kati yao wa kike wakiwa 382 na wa kiume 892
Wilaya ya Uyui imewatambua watoto 1,946 ambao wanaishi katika
mazingira hatarishi.


Katika kukabiliana na tatizo hilo wilaya ya Nzega kwa kushirikiana
na Wizara ya kazi na ajira imeunda kamati ya ufuatiliaji ya watoto
wanaotumikishwa kwenye mashamba ya tumbaku.


Kwa upande wa manispaa ya Tabora imeunda kamati ya kukomesha
utumikishwaji wa watoto ambayo itakuwa na jukumu la kupita vijijini
kutoa elimu juu ya madhara ya ajira kwa watoto huku  wilaya ya
Kaliua kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ikiomba shilingi milioni 19 ili
kutekeleza zoezi hilo



Na Fredy Hangaya-Tabora

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.