MTANGAZAJI

UNDP YATOA MSAADA KWA TANAPA IRINGA

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) mkoani Iringa  limepokea msaada wa magari matatu aina ya Toyota Pickup na greda moja kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na miundombinu ya barabara.

Msaada huo umetolewa kupitia Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) ambapo Hati za makabidhiano zilisainiwa jana huku upande wa UNDP ukiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi Mkaazi wa UNDP nchini , Mandisa Mashologu na TANAPA ikiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dk Ezekiel Demba.


Kwa kupitia msaada huo, Mratibu wa SPANEST, Godwel Ole Meing’ataki amesema hifadhi ya Taifa ya Ruaha imepata greda na magari mawili huku Hifadhi ya Kitulo ikiondoka na gari moja.


Msaada wa magari hayo utasaidia kupunguza changamoto inayowakabili askari wanyamapori katika kukabiliana na ujangili huku greda hilo likitumika kuimarisha miundombinu ya barabara katika hifadhi na vijiji jirani.


Na:Isaya Mdahila-Iringa

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.