MTANGAZAJI

TAKUKURU WAMSHIKILIA MWEKA HAZINA WA MANISPAA YA MUSOMA KWA TUHUMA ZA KUDAI RUSHWA YA NGONO

Taasis ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Mara(TAKUKURU)
inamshikilia mweka hazina wa Manispaa ya Musoma Livingstone Kahwa
kwa tuhuma za kudai rushwa ya ngono kutoka kwa msichana anaefanya
mafunzo kwa vitendo katika idara ya fedha ya halmashauri hiyo.

Kaimu  mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara  Ferouz Korongo  amesema kuwa
mtuhumiwa alikamatwa akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Givalen
Motel chumba namba kumi, majira ya saa 1:20 Februari 24 mwaka huu
wilayani Butiama.

Korongo alisema kuwa awali walikuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa
mlalamikaji kuwa alikuwa amefanya kazi ya ukaguzi wa leseni za
biashara katika muda wa ziada ambapo alikuwa ameidhinishiwa kulipwa
kiasi cha shilingi 40,000,ambapo mweka hazina huyo alimtaka atoe
rushwa ya ngono ili aweze kupa kiasi hicho cha fedha.

“Huyo msichana alipoona anadhalilishwa,na pia anaonewa kupewa haki
yake,ilimladhimu kufika katika ofisi zetu kutoa taarifa,ambapo
tulimwelekeza namna ya kufanya ili tuweze kumtia mtuhumiwa
hatiani”amesema Korongo.

Amesema kuwa Takukuru waliandaa mtego ambapo mtuhumiwa alifika
katika eneo la Kamnyonge siku hiyo majira ya saa 11:15 jioni katika
eneo alilokuwa amempigia simu mlalamikaji kuwa wakutane katika eneo
hilo ambapo alimtaka mlalamikaji kuingia katika gari aliyokuwa nayo
mtuhumiwa Toyota Rav 4 lenye namba za usajili     T176 BKU.

Korongo alidai kuwa hapo ndipo mtuhumiwa alipoendesha gari hiyo
hadi katika wilaya ya Butiama maeneo ya Makutano Mmazami katika
nyumba hiyo ya wageni na kufanikiwa kuchukua chumba,ambapo
walimnasa kabla hajamdhuru mlalamikaji.

Na.Mohamedi Nyabange

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.