TAMWA YAWAPONGEZA WANAHABARI UANDISHI WA HABARI ZA UKATILI WA KIJINSIA
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka akizungumza na wahariri na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Makao Makuu ya Ofisi hizo, Sinza Jijini Dar es Salaam. |
![]() |
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwa katika mkutano huo |

![]() |
Mmoja wa wahariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Lilian Timbuka (wa kwanza kushoto) akichangia mada katika mkutano huo. |
Bi. Nsoka ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akiwasilisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa mradi wa GEWE
II (Mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya
wanawake na watoto) kwa wahariri na waandishi wa habari waandamizi
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Alisema kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2012 hadi
Septemba 2013, jumla ya habari 499 ziliandikwa kwenye magazeti
mbalimbali kupitia mradi wa GEWE, huku habari 216 zikiandikwa kwenye
miradi mingine ya taasisi hiyo hivyo kufanya idadi ya habari zote
kufikia 715 kwa mwaka.
Alisema ongezeko hilo limeleta mafanikio kadhaa kwa
jamii hivyo kuwaomba waandishi wa habari waongeze juhudi za uandishi wa
habari za ukatili wa kijinsia ili kukomesha vitendo hivyo vinavyo
endelea kuiathiri jamii.
"...Hali inaonesha uchapishaji wa habari uliongezeka
zaidi kwa vitendo vya ukatili, ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2012
ambapo uchapishaji wa habari katika magazeti ulikuwa na Idadi ya 350 kwa
miradi yote ya TAMWA," alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema ongezeko hilo la uandishi wa habari za
ukatili wa kijinsia limeleta mafanikio kwa kiasi fulani, kwani kwa sasa
jamii imepata uelewa kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na waliokuwa
wakinyanyasika sasa wamejitokeza kuomba msaada zaidi.
"...TAMWA imekua ikipokea simu kutoka sehemu
mbalimbali za Tanzania watu wakiomba msaada wa kutatuliwa matatizo yao.
Kituo ha usuluhishi cha TAMWA kimekua kikipokea watu wakisema wamepata
habari baada ya kusoma au kuona machapisho au tangazo kupitia luninga au
kusikiliza redio...," alisema Bi. Nsoka.
Aidha alisema waandishi wa habari wa Dar es salaam
na mikoa mingi sasa wameweza kuandika na kutangaza habari mbalimbali za
ukatili wa kijinsia kwa ufasaha.
Akizungumzia
matokeo ya utafiti wa kihabari uliofanywa na TAMWA kwa kushirikiana na
waandishi wa habari, alisema utafiti ulibaini kuwa asiliamia 17 ya
wananchi hawana uelewa wa sheria za ukatili wa kijinsia, huku Mkoa wa
Lindi kupitia Wilaya ya Lindi Vijijini ikiongoza kwa kupata asilimia 12.
Alisema utafiti huo uliowahoji jumla ya watu 2,300
pia ulibaini kuwa asilimia 47 za kesi huripotiwa katika Serikali za
vijiji na asilimia 25 huripotiwa katika vituo vya polisi. Utafiti
ulinesha kuwa wananchi hawana majukwaa ya kukaa pamoja na kujadili
changamoto zao ambapo ni asilimia 13.5 ndiyo wanachama wa asasi za
kijamii.
TAMWA kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya
habari kiliwatuma waandishi wa habari kwenda katika Wilaya 10 za mradi
na kufanya utafiti ambao matokeo yake yalitolewa mwezi Julai 2013.
Wilaya 10 za Tanzania Bara na Visiwani, ni pamoja na Kinondoni, Ilala,
Kisarawe, Mvomero, Ruangwa, Lindi Vijijini, Newala, Wete, Unguja Mjini
Magharibi na Unguja Kusini.
Chanzo:www.thehabari.com
Post a Comment