TAARIFA YA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUHUSU MGOMO WA WAFANYABIASHARA
Mamalaka ya Mapato
Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wafanyabiashara kwa ujumla
Kuwa inasikitishwa na mgomo wa wafanyabishara kwa kufunga maduka maeneo mbali
mbali nchini.
Ifahamike kuwa
Matumizi ya mashine ya EFD ni jambo la kisheria na lilipitishwa na bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2011.
Pamoja na sheria
kupitishwa, viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko kwa nyakati tofauti
kwa kuanzia na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Machi 2011.
Pia Makamu wa Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Billal alikazia jambo
hili tarehe 8 Mwezi November mwaka 2013.
Waziri mkuu wa
Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alilitolea tamko pia
Mwezi Desemba 2013 wakati akiahirisha Bunge kwa kusisitiza msimamo wa serikali
kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi wa mashine za EFD.
Tarehe 29 Januari
2014, Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya Salum aliweka bayana msimamo wa Serikali
kwa kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni swala la kisheria na
litaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa
nyongeza kwa wafanyabishara kununua mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014
baada ya kuongeza muda mara tatu kwa nyakati tofuati.
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) pia kwa nyakati tofauti na maeneo tofuati imelitolea tamko jambo
hili na itaendelea kufanya hivyo.
Kwa masuala ya
kiutendaji yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi
ikiwemo utoaji wa Elimu kwa umma.
Mamlaka ya Mapato
Tanzania inapenda kuwafahamisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa watu
wanaolazimisha wafanyabishara wenzao kufunga maduka kwa kuwatishia na
kuwashurutisha wanavunja sheria kwa kusababisha uvunjifu wa amani nchini na
hivyo mkono wa sheria utawafikia.
Pia imefahamika
kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa bali
hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya TRA imekuwa ikipokea taarifa
na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara na wananchi wema wakiomba ulinzi
ili wafungue maduka yao na kufanya biashara maana ndio ajira yao na mahali
pakujipatia riziki ya kila siku.
Ifahamike kwamba
wale wote wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja sheria kwa kuwalazimishwa
wafanyabiashara kugomea agizo halali la kisheria hivyo kwa wale wote
wanaotishiwa au kushurutiswa watoe taarifa kwa kupiga simu namba zifuatazo 0786 800
000, 0713 800333, 0800
110016 au barua pepe info@tra.go.tz
“PAMOJA TUNAJENGA
TAIFA LETU”
IMETOLEWA NA KAIMU
KAMISHNA MKUU
MAMLAKA YA MAPATO
TANZANIA
Post a Comment