MORNING STAR TELEVISHENI YAPATA KIBALI CHA KURUSHA MATANGAZO
Mkurugenzi
wa Vyombo vya Habari wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania
Mchungaji Musa Mika (pichani) jana mchana kupitia radio ya Morning star
ametangaza rasmi kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa
Kanisa hiyo kibali cha kurusha matangazo ya Televisheni tarajiwa ya
Morning Star.
Mchungaji
Musa Mika pia amesema uzinduzi wa Morning Star Televisheni utafanyika
hivi karibuni na wakati ukifika watatangaza king'amuzi kitachokuwa
kinarusha matangazo ya kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la
Waadventista wa Sabato Tanzania.
Mchungaji
Mika pia alichukuwa fursa hiyo kwa kuwashukuru waumini wa kanisa hilo,
wapenzi wa radio ya Morning Star na watanzania wote kwa ujumla kwa kuwa
pamoja nao katika sala kwa muda mrefu wakati wakisubiri habari njema
kama hii.
Chanzo:chingaone
Post a Comment