MTANGAZAJI

MTANGAZAJI WA EAST AFRICA TV KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA

Marehemu Ken Kidago

Habari za hivi punde zilizoifikia blog hii ni kwamba Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa, Ken Kidago amefariki dunia.

Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken  hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la  polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua  kabidi wavunje na kuingia na kukuta  amefariki.

Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.

Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha kujiunga na Tripple A FM ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.