MTANGAZAJI

GM VIDEO CENTER YAKABIDHI ZAWADI YA LULU ZA INJILI KWA MSHIKAMANO SDA CHOIR


Felix Mark Makachayo
Kampuni ya  GM Video Center ya jijini Dar es salaam imekabidhi hii leo Biblia kumi kwa kwaya ya Mshikamano SDA ya Meatu mkoani Simiyu ambazo ni zawadi kwa kwaya hiyo kutokana na wimbo wake wa Yusufu wa Leo, kuwa wimbo wa mwaka katika kipindi cha Lulu za Injili kinachosikika saa 11 jioni katika kituo cha Radio cha Morning Star kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania.

Wimbo huo uliopo katika video yao namba tatu ulipata nafasi hiyo mwaka 2013/14  kutokana na kupigiwa kura na wasikilizaji wa kipindi cha Lulu za Injili waliopigia kura kwa kila wimbo wa mwezi katika mwaka mzima.

Mwalimu wa kwaya ya Mshikamano Felix Mark Makachayo ndiye amekabidhiwa Biblia hizo hii leo jijini Dar es salaam.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa kwaya hiyo ambayo ina matoleo matatu ya video kwa wimbo wake kuchaguliwa kuwa wimbo wa mwaka wa kipindi cha Lulu za Injili ambapo mwaka 2012/13  ilipata nafasi hiyo kwa wimbo wake wa Mguso ulipo katika video nambari mbili kuwa wimbo wa mwaka .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.