TUZO YA JAMII KUTOLEWA MWAKA HUU
Jamii Kwanza Kuzindua Tuzo ya Jamii mwezi Juni,2014.
Kampeni ya Jamii Kwanza inatarajia kuzindua Tuzo ya Jamii ifikapo mwezi Juni 2014.
Mmoja wa viongozi wandamizi wa Jamii Kwanza Mwanasheria Amani Mwaipaja ameiambia blog hii kuwa Tuzo ya Jamii itatolewa kwa watu binafsi (Individuals) ambao wanatumia muda, Elimu, nguvu na Rasilimali zao katika kusaidia, kutumikia, na kuhudumia Jamii.
Tuzo ya Jamii inaratibiwa na Kampuni ya Tanzania Awards International Limited iliyosajiliwa kisheria na Msajili wa Makampuni Nchini Tanzania. Tanzania Awards International Limited ni kampuni inayojihusisha na masuala ya Utafiti, Ushauri wa Kitaalam (Consultancy) na Uratibu wa Matukio ikiwemo utoaji wa Tuzo za Kimataifa.
Post a Comment