MTANGAZAJI

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA OMAR SKYES HUKO WASHINGTON DC,MAREKANI

Eneo la tukio Washington DC ambapo Omar Sykes (picha ya ndani) aliuawa.
Photo Credits: National Review Online
Jumanne wiki hii, idara ya Polisi Washington DC (Metropolitan Police Department) ilitangaza kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja kati ya wawili waliokuwa wakitafutwa kwa mauaji ya mwanafunzi mtanzania aliyekuwa akisoma katika chuo kikuu cha Howard hapa jijini.
Omar Sykes (22) aliuawa usiku wa Julai 4 mwaka huu nje kidogo ya maeneo ya chuo hicho alipokuwa pamoja na mwenzake.
Wakiwa mtaa mmoja toka chuoni, wanafunzi hao walivamiwa na watu wenye silaha waliotaka kuwapora, na katika harakati hizo, Omar alipigwa risasi kifuani na kufariki.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 19, 2013

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.