MTANGAZAJI

JULIUS NYAISANGA "UNCLE J"AFARIKI DUNIA

 
Marehemu Julius Nyaisanga wakati wa uhai wake
Kutoka kushoto kwenda kulia,Richard Maabadi,Sauda Simba,Rukia Mtingwa,Manambi Ismail
Uncle J Julius Nyaisanga (Marehemu)John Ngahyoma (Chanzo:bongocelebrity.com)

Habari zilizoifikia blog hii na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro,Aziz Msuya kwa njia ya simu toka mjini humo zinaeleza kuwa mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Julius Nyaisanga 'Uncle J" amefariki dunia  leo asubuhi katika hospitali ya Mazimbu iliyoko katika Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) eneo la Mazimbu alikokuwa amelazwa.
Msuya ameeleza kuwa Mwili wa Marehemu utahamishiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro asubuhi hii kwa ajili ya taratibu zingine.
Nyaisanga alikuwa ameshaomba likizo ya mapumziko kutokana na kutoka Radio Aboud ambako alikuwa akifanyakazi kutokana na kuugua



Kwa mujibu wa chanzo chetu taarifa za kifo chake zimezagaa asubuhi hii na bado haijafahamika zaidi sababu za kifo chake



Julius Nyaisanga  alijulikana sana tangu akifanya kazi Redio Tanzania sasa hivi inajulikana kama TBC Taifa,ITV na Redio One stereo kabla ya kwenda Morogoro kujiunga na Radio Aboud.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.