MTANGAZAJI

MADAWA YA KULEVYA BADO NI TATIZO KUBWA NDANI YA JAMII



Miongoni mwa habari inayoonekana kujadiliwa sana katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari hapa nchini Tanzania na nje ya nchi  ni ile inayowahusu wanawake wawili wanaotajwa kuwa ni watanzania ambao wanatuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika ya Kusini.Pamoja na kukamatwa kwa wanawake hao bado suala hili linaonekana kushika kasi hapa nchini Tanzania.

Takwimu za jeshi la polisi Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini Tanzania zinaonesha kuwa walikamata dawa za kulevya za aina mbalimbali zenye uzito wa kilo 55,285 katika maeneo tofauti ya nchini humo tangu Januari hadi Desemba 15, mwaka 2012

Kukamatwa huko kulikwenda sambamba na kunaswa watu 6,929 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo ya mihadarati, huku idadi kubwa ikiwa ni wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 40.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema hali hii inaonyesha wazi kuwa, wanawake wanashiriki kikamilifu katika kusafirisha dawa hizi.

Alisema hataki  kuzungumzia mtandao kama ni wa vigogo au watu wa kawaida, kikubwa anachokifanya ni kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

 Kamanda Nzowa alisema dawa za kulevya aina ya cocaine zilikamatwa kilo 151, heroine (260), bangi 48,658 na mirungi kilo 6,216.

Kamanda Nzowa alisema baadhi ya dawa hizo zinaingizwa na Watanzania wenyewe kutoka nchi za nje na nyingine na raia wa kigeni kwa ajili ya kuziuza au kuzipeleka katika masoko mengine ya nje.

Takwimu za ukamataji  kutoka Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2010 hadi Mei 2013 jumla ya kilo 742.5 za heroin, kilo 348.3 za cocaine, kilo 77.740 za bangi na kilo 16,334 za mirungi zilikamatwa.

Alisema maeneo yanayotumika kusafirishia dawa hizo ni katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Pia alisema, wahusika wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za panya kuingiza dawa hizo nchini, ambapo alisema wamefanikiwa kudhibiti maeneo mbalimbali ikiwamo viwanja vya ndege na bandari, lakini hawa jamaa ni wajanja na wamebadilisha njia za kuingiza dawa hizo nchini. na jeshi hilo linaendelea  kupambana kwani baada ya kubana huku (bandari na viwanja vya ndege), wakabaini  wanatumia bandari ndogo ya Bagamoyo, Mnazi Bay ya Mtwara kwa kuingiza au kusafirisha.

Kamanda Nzowa alisema katika kipindi hicho  kulikuwa na kesi  29  Mahakama Kuu na watu 138 walituhumiwa kukutwa na cocaine, wakati 400 walikutwa na heroine.
Ambapo kesi zingine zilikuwa katika Mahakama za kawaida ambako watu 5,544 likuwa wanatuhumiwa kukutwa na bangi na 847 mirungi, 

Nzowa alisema jeshi la pilisi limejipanga  kikamilifu kwa mwaka 2013 na zaidi ni kuhakikisha wanadhibiti maeneo yote yanayotumika kuingiza au kupitisha dawa hizo na wameweka mitego katika njia zote za panya na wakiwakamata wahusika watawaafikisha mahakamani,

--



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.