ZAWADI YA KUREKODI ALBUM BURE KWA WAIMBAJI WA INJILI TOKA KWA MTANGAZAJI HII HAPA
Kampuni ya Excellent Pro ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na kipindi cha Lulu za Injili na Acappella vya Morning Star Radio wanakuletea zawadi mwimbaji/waimbaji wa nyimbo za injili zawadi nyingine mwaka huu wa 2013 yaani GOSPEL OFFER MWAKA 2013.
· Lengo
la Gospel offer 2013 ni kuchangia/kusupport juhudi zinazofanywa na wasanii
(Kwaya za kanisa, Vikundi binafsi na Mwimbaji mmoja mmoja) katika kutambua
vipaji.
· Gospel
Offer 2013 inadhaniniwa na kipindi cha Lulu za Injili na Acappella kwa
kushirikiana na Excellent Pro.
·
Gospel
Offer 2013 inadhamilia kurekodi albam 1 ya nyimbo mpaka 12 kwa kwaya na 10 kwa
vikundi na mwimbaji binafsi.
·
Kumbuka kuwa
Gospel offer ya 2012 ilimpatia zawadi Angel Magotti kurekodi wimbo mmoja bure
· Makundi
yanayokusudiwa kuingia katika mchakato wa kupata mshindi katika Gospel offer
2013 ni kwaya za kanisa, vikundi na mwimbaji binafsi.
· Kwaya,
vikundi au mwimbaji binafsi atagharimiwa gharama za kurekodi katika mojawapo ya studio zilizopo Dar es
salaam. Usafiri, chakula na gharama zingine ni wajibu wa kwaya, kikundi au
mwimbaji binafsi.
· Mchakato
wa kumpata mshindi atakayenufaika na Gospel Offer 2013 utachukuwa mwezi mmoja;
na tukio la kurekodi litakuwa mwezi wa tisa 2013, ili kutoa muda muafaka kwa
maandalizi ya mshindi kufanya vizuri.
VIGEZO (CRITERIA)
·
Ni
kwaya, vikundi na waimbaji binafsi wa nyimbo za injili tu.
·
Kwaya,
vikundi na waimbaji binafsi ambao watakuwa na mipango madhubuti ya kufanya
recording tu. Mchakato wa kuchuja
utawaengua ambao hawatakuwa na dhamira za dhati kurekodi.
·
Kwaya,
vikundi au waimbaji binafsi wanaoibuka watapata kipaumbele.
·
Mshindi
atapatikana kwa kupigiwa kura nyingi na wasikilizaji wa kipindi cha Lulu za
injili.
·
Mwakilishi/mhusika
wa kwaya, kikundi au mwimbaji binafsi yoyote ana nafasi ya kupendekeza jina la
kwaya, kikundi au mwimbaji binafsi.
· Pendekeza
jina la kwaya, kikundi au mwimbaji binafsi tuma ujumbe wa simu GO……….kwenda
namba 15551………….
· Pigia
kura kwaya unayopenda kuwa mshindi wa Gospel offer 2013 tuma ujumbe wa simu GO….
Kwenda namba 15551………….
·
(
July 7 – 13, 2013) – Kuzindua Gospel Offer 2013
·
(Julai
14 – 20, 2013) – Majina ya Kwaya, vikundi na waimbaji binafsi kupendekezwa kwa
ujumbe wa simu.
·
(Julai
21 – 27, 2013) – Kuchuja kwaya zibaki 5, vikundi 2 na waimbaji binafsi 2 na
kuwatangaza.
·
(
Julai 28 – Agasti 3, 2013) – Wasikilizaji wa Lulu za injili/Acappella kupiga
kura kwa ujumbe wa simu.
·
(Agasti
4 – 10, 2013) Wasikilizaji wa Lulu za injili/Acappella kupiga kura kwa ujumbe
wa simu.
·
(Agasti
11 – 17, 2013) kufanya tathimini ya kura za wasikilizaji wa Lulu za injili
/Acappella kutangaza washindi wawili (Kwaya moja na Kikundi/mwimbaji binafsi)
·
(Agasti
17 – 31, 2013) Washindi kujiandaa na mazoezi kwa ajili ya kurekodi.
·
Septemba
1, 2013 – Kwaya kurekodi
·
Septemba
8, 2013 – Kikundi/au mwimbaji binafsi kurekodi
·
Septemba
9 – 14, 2013 Kazi ya kwaya mshindi kutamburishwa
·
September
15 – 21, 2013 Kazi ya kikundi/mwimbaji binafsi kutambulishwa
·
Septemba
22 – 28, 2013 Kuwapa pongezi washindi katika vipindi vya Lulu za
injili/Acappella
Post a Comment