MTANGAZAJI

KONGAMANO LA WAZI LA MPANGO TOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

 
 
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Mada kuu ni kujadili, kushauri na kutoa maoni juu ya miradi mikubwa ya kitaifa ya sekta ya nishati itakayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu, Julai 2013 – Disemba 2015 ili kuliwezesha Taifa kufikia Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

Wadau wanaoalikwa ni pamoja na:

Mabenki washirika, Wakandarasi kwenye sekta ya Umeme, Wahandisi kutoka Taasisi na Vyuo Vikuu nchini, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Wawakilishi kutoka Makampuni mbalimbali, Migodi, Viwanda vikubwa na vidogo na wananchi wote kwa ujumla.

Hakuna kiingilio kwenye uzinduzi huo.

“Matokeo Makubwa sasa kwa maendeleo ya Mtanzania”

Imetolewa na:
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.