MTANGAZAJI

TAARIFA KUHUSU KUPIGWA RISASI KWA MHARIRI WA GAZETI

BUSINESS TIMES LIMETED

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KUVAMIWA NA KUDHURIWA KWA MHARIRI WA BUSINESS TIMES, MNAKU MBANI


AGOSTI mosi mwaka huu, Mhariri wa Gazeti la Business Times linalotoka

mara moja kwa wiki (kila Ijumaa), alijeruhiwa kwa risasi akiwa njiani
kurudi nyumbani kwake Mbagala, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea saa mbili usiku, eneo la Mtoni Madafu, akiwa

katika gari binafsi aina ya Noah inayomilikiwa na Bw. Mgeme Singili
(namba ya gari imehifadhiwa) na abiria wengine wakitokea Kariakoo
kwenda Mbagala.

Walipofika Mtoni Mtongani, gari hiyo ilisimamishwa na majambazi sita

waliokuwa katika pikipiki. Majambazi hao walichomoa funguo ya gari na
kudai wapewe begi lenye pesa kutoka kwa mmoja wa abiria waliokuwa
ndani ya gari hiyo.

Abiria waliwajibu hakuna mtu mwenye begi la pesa ndipo majambazi hao

walipoanza kufyatua risasi mfululizo (zisizo na mwelekeo), wakiwalenga
abiria ndipo moja kati ya risasi hizo ilimpata Bw. Mnaku Mbani.

Bw. Mnaku alipigwa risasi juu ya mdomo, upande wa kulia ikatoke kwenye

shavu la kushoto. Risasi hiyo iliondoa meno matatu ya juu.
Uongozi wa kampuni umezungumza na Bw. Mnaku ili kuelezea mazingira ya
tukio hilo lakini kutokana na maumivu aliyonayo, hatukuweza kuzungumza
naye kwa kirefu.

Hali ya Mnaku inaendelea kuimarika na anendelea kupata uchunguzi wa

madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zaidi ya jeraha hilo,
Mnaku hana majeraha mengine katika mwili wake kutokana na tukio hilo.

Uongozi wa Makampuni ya Business Times Limited unaendelea kufuatilia

hali ya Mnaku kwa karibu ili kuhakikisha anapata huduma na uangalizi
unaostahili.

Taarifa Za Polisi

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime alisema mmiliki wa
gari hiyo ni mfanyabiashara ambapo uchunguzi wa polisi umebaini kuwa
majambazi hao waliamini kuwa amebeba pesa, hivyo baada ya kushuka
kwenye pikipiki walidai kupewa pesa.

Alisema katika gari hiyo watu watatu walijeruhiwa kwa risasi akiwemo

Bw. Mnaku, mwingine katika bega la kushoto na watatu alikwaruzwa na
risasi kisogoni.

Chanzo:wanabidii

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.