MTANGAZAJI

IKULU YA TANZANIA ILIVYOKANUSHA HABARI KUWA RAIS HAKUTOFAUTIANA NA WAZIRI MKUU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili  mjini Blantyre ,Malawi  jana jioni  kuhudhuria  Mazishi ya Profesa Bingu  wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi., aliyefariki tarehe 5 April, 2012  Kufuatia matatizo ya Moyo

Rais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi jirani na Malawi.

Nchi hizo ni Afrika Kusini, Benin, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia.

Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.

Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.
Pia  nitumie nafasi  hii kuwatahadharisha waandishi wa habari  kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.

Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.

Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea Bungeni.

Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.

Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu , bali  hata viongozi na wananchi kwa ujumla.

Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho  tarehe 23 April mara baada ya maziko..

Mwisho ..................


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Blantyre -Malawi.
22 April, 2012


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.