MTANGAZAJI

TAARIFA YA MADAKTARI YA KUSITISHA MGOMO

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012.
Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda
kutoa ufafanuzi ufuatao:

... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya

kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii
(social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi
(Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi

anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi
hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha
maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini

lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa
yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya

faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini
na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na
dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha

na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:


JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO

WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU,
AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI
SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA

TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA
RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA

IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA
KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU

WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA
HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA
KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.

RAIS(MAT)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.