MTANGAZAJI

MAANDAMAANO YA WANAHARAKATI JANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, Dr. Hellen Kijo-Bisimba akizungumza vyombo vya habari










Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, jana walishirikiana na asasi mbalimbali za kiraia, waliandaa maandamano ya amani saa tisa mchana, kuanzia Salendar Bridge. 

Maandamano hayo yalikuwa na lengo la  wapenda amani na wapenda haki, kuungane nao kutuma ujumbe kutaka Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Mganga Mkuu Wizara ya Afya wafutwe kazi mara moja; madaktari warudi kazini mara moja; serikali na madaktari wakae meza moja na kujadili masuala muhimu ya afya, na wafikie makubaliano ndani ya miezi mitatu.

Hii leo  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, Dr. Hellen Kijo-Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria, na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya na wanaharakati wengine 13 wamekamatwa na polisi, na kupelekwa  kituo cha Polisi Oysterbay  kwa tuhuma za kutaka kusababisha uvunjifu wa amani kutonakana na maandamano yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.