TAHADHARI KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM,TANZANIA
Gazeti la NIPASHE toleo la leo limeandika kuwa wakazi wa jiji la Dar es salaam nchini Tanzani wapo hatarini kula samaki wenye sumu baada ya kampuni moja (jina linahifadhiwa)kudaiwa kuingiza shehena ya samaki hao wanaodaiwa kuwa na mionzi ya nyuklia.
Habari za uhakika ambazo NIPASHE jumapili imezipata ni kwamba shehena hiyo ya samaki iliingizwa nchini wiki tatu zilizopita na kapuni hiyo ya jijini kutoka nchini Japan kupitia bandari ya Dar es salaam.
Watoa habari hizo wamesema samaki hao walikuwa wamehifhadhiwa kwenye kontena tano zenye uzito wa tani 25 kila moja.
Aidha taarifa hizo zinaeleza samaki hao wametokea mji wa Fukushima ambapo maji ya bahari yaliyozunguka mji huo wameathiriwa na mionzi ya nyuklia iliyotokana na kulipuka kwa vinu vitatu vya mionzi.
Post a Comment