MTANGAZAJI

WACHINA WATENGENEZA MAZIWA YA BINADAMU TOKA KWA NGO'MBE

Wanasayansi wa nchini China wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa kama yale yanayotolewa na wanawake wanaonyonyesha. Wanasayansi wa nchini China wametamba kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe 300 wanaotoa maziwa kama ya BINADAMU.

Katika ripoti ya wanasayansi hao iliyotolewa kwenye jarida la Public Library of Science One journal, wanasayansi hao walisema kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa yenye protini ya Lysozyme ambayo hupatikana kwenye maziwa ya binadamu pekee ambayo humwezesha mtoto kuweza kujilinda na maradhi mbalimbali.


Wanasayansi hao waliifanyia marekebisho embryo ya ng'ombe na kisha kuipandikiza mimba kwenye ng'ombe jike ambaye alipozaa alizaa ng'ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kama ya binadamu.
  



 "Maziwa haya ni tofauti kabisa na maziwa ya kawaida ya ng'ombe, yana ladha tofauti na maziwa ya ng'ombe", alisema Profesa Ning Li, kiongozi wa utafiti huo katika chuo kikuu cha China Agricultural University.

"Tuna malengo ya kuuza baadhi ya tafiti za ugunduzi huu ndani ya miaka mitatu ijayo", alisema Profesa Ning Li na kuongeza " Itachukua kama miaka 10 kabla ya watu hawajaanza kununua maziwa ya binadamu madukani".


Profesa Li aliongeza kuwa maziwa hayo yatakuwa na virutubisho vingi muhimu kwa mwili wa binadamu.


Hata hivyo utafiti huo umewagawanya watu ambapo baadhi wanaupinga huku wengine wakiuunga mkono.


"Tuna wasiwasi mkubwa na utafiti huu wa kuwafanyia marekebisho ng'ombe na kuwapandikiza vinasaba vya binadamu", alisema Helen Wallace, mkurugenzi wa GeneWatch UK.


"Kuna maswali mengi kama maziwa haya yatakuwa salama kwa binadamu, inabidi yafanyiwe majaribio makubwa kama majaribio yanayofanywa kwa madawa katika kuchunguza kama yatakuwa hayana madhara kwa binadamu", aliongeza bi Helen Wallace.


Hata hivyo Profesa Keith Campbell, mtaalamu wa baiolojia katika chuo kikuu cha University of Nottingham nchini Uingereza amepingana na bi Helen na kusema kuwa kama taratibu zote za kitaaluma kuhusiana na vinasaba zitatumika maziwa hayo hayatakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.
 
Toka: NIFAHAMISHE

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.