MTANGAZAJI

KAZI ZAIDI YA MASAA 11 KWA SIKU HATARI KWA MOYO WAKO

Wale wanaofanya kazi kwa zaidi ya masaa kumi na moja kwa siku wana hatari kubwa ya kukumbwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Utafiti uliofanywa na watafiti wa taasis ya University College of London wanasema theluthi mbili ya watu wa aina hii wana nafasi ya kusumbuliwa na magonjwa ya moyo baadae.
 
Watafiti hawa wanasema kufanya kazi kwa masaa mengi bila kupumzika ni mchango mkubwa sana katika vitu vinavyosababisha matatizo ya moyo ukiacha unywaji pombe na uvutaji wa tumbaku.

Utafiti huu ulitafiti watu 7,000 ambao walikuwa ni waajiriwa wa serikali ya Uingereza katika taasis ya Whitehall, na ulifanyika kwa kipindi cha miaka 11 ukizingatia masaa ambayo watu hawa walikuwa wanatumia kwenye kufanya kazi zao za kila siku.

Wakati huo huo watafiti hawa walikuwa wakikusanya historia za kiafya kwa upande wa moyo za wafanyakazi hao kutoka katika hospitali ambazo watu hawa walikuwa wakienda kwa uchunguzi wa kiafya.

Katika kipindi hicho cha miaka 11 watu 192 kati ya 7,000 ya waliokuwa wakifanyiwa utafiti huu walipatwa na mshtuko wa moyo. Asilimia 67 ya watu hawa 192 waligundulika kufanya kazi zenye msongo mkubwa kwa zaidi ya masaa 11 ya kazi kwa siku, tofauti na wale waliokuwa wakifanya kazi kuanzia saa tatu asubuhi na kufunga kazi zao saa kumi na moja ya jioni (au masaa nane kwa siku).

"Utafiti wetu umehitimisha kwamba kufanya kazi kwa masaa mengi zaidi ya mwili unavyomudu kunahatarisha zaidi mtu kupatwa na mshtuko wa moyo" Anasema Profesa Mika Kivimaki, kiranja mkuu wa utafiti huu.

"Huu ni wito wetu kwa watu wanaofanya kazi kupindukia (workaholics), hasa kama watu hawa tayari wanafanya mambo mengine yanayohatarisha kupatwa na mshtuko wa moyo kama uvutaji wa tumbaku na unywaji wa pombe." anaongeza Profesa Kivimaki.

Utafiti huu umechapishwa katika jarida la kitabibu la Annals of Internal Medicine.

Kutoka:FOTOBARAZA

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.