MTANGAZAJI

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mfanyabiashara wa kuuza mkaa katika Manispaa ya Morogoro akikokota baiskeli huku akiwa amebeba mkaa kwenye mkaa wakati akielekea katikati ya mji huo kwa ajili ya kutafuta wateja wake ambapo kiroba kimoja huuza kati ya 2000 hadi 2500.picha toka http://www.jumamtanda.blogspot.com/

1 comment

Anonymous said...

Mtangazaji. Naona hapa umekurupuka tena kama ilivyo kawaida yako na sioni uhusiano wa hii picha na mada yenyewe. Ina maana Tanzania haipaswi kuwa na wauza mkaa? Ni wapi ambako hakuna masikini au watu wenye shida na kazi ngumu kama hizi? Nenda jijini Los Angeles nchini Marekani ukaone. India? China? Uingereza?

Kukurupuka kama huku bila kutoa mawazo na uchambuzi wa kina kuhusu matatizo yanayoikabili jamii pamoja na MASULUHISHO yake ni dalili ya kutokomaa kifkra au kutokutazama mambo kwa jicho pana. Vinginevyo pengine ni bora tu utushushie Historia ya Ellen G. White au mitazamo mbalimbali katika theolojia ya msingi katika maandiko yake. Tutafaidika sana!

Unayo tabia ya kubania comments zenye mawazo endelezi. Hata hii ukiibania ni sawa lakini naamini kwamba ujumbe umefika.

Mtazamo News . Powered by Blogger.