MTANGAZAJI

TAARIFA KWA WATANZANIA WAISHIO KANADA

Kwa niaba ya Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, naomba kuchukua fursahii kuwajulisha kuwa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Kimataifa anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchiniCanada kuanzia tarehe 11 Januari hadi 15 Januari, 2010.

Akiwa Ottawa Mhe. Waziri Membe atapenda kukutana na Watanzania waliokoCanada. Ubalozi unafanya utaratibu wa kupata ukumbi kwa ajili yamkutano huo ambao utafanyika siku ya tarehe 12, Januari, 2010 jionisaa Kumi na Mbili na Nusu hadi saa Tatu na Nusu usiku (6:30Pm-9:30Pm).

Tutawajulisha sehemu ya mkutano na anuwani ya shughuli hiyo kabla yamwisho wa juma hili hivyo tunaomba muweke shughuli hii katika ratibazenu.

Aidha, tunaomba kila atayepata ujumbe huu atusaidie kumjulisha/kuwajulisha Watanzania wenzetu ambao hatukuweza kuwatumiabarua pepe hii kutokana na kutokuwa na anuwani zao.

Kama mnavyojua shughuli ni watu na watu ndiyo sisi sote hivyo tunaombatujitokeze kwa wingi kuja kukutana na Mhe. Waziri Membe ambaye kamawengi mnavyokumbuka aliishi hapa Ottawa wakati akifanya kazi kwenyeUbalozi wetu huu.

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu,Kny Balozi

Pauline Mengi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.