MTANGAZAJI

KERO KWA POLISI WA TANZANIA

Katika mambo mimi yananikera Tanzania hii ni kuona mtu aliyeua jambazi anaonyeshwa hadharani lakini jambazi lililowawa au kukamatwa au kukimbia kwamba linatafutwa halionyweshwi. Sasa namna hii tutamaliza ujaambazi namna gani?.
Kwa nini mtu jambazi anakamatwa lakini tunaonyweshwa silaha peke yake?.

Kwa nini tusionyeshwe Jambazi lenyewe ili sisi Raia wema tusaidie Polisi kuwataja watu walio na mahusiano na Jambazi huyo.

Mimi naona ni makosa kumuonyesha Askari aliyeua Majambazi kwani tunamhatarishia usalama wake. Anayepaswa aonyeshwe hadharani ni Jambazi ili watu waweze kuwataja watu wenye mahusiano ya ujambazi au ya biashara na mtu yule.

Jeshi la Polisi naombeni badilini utaratibu wenu wa kuficha sura za wahalifu. Itasaidia kupunguza uhalifu kama mtaweka wazi sura za watu hawa.

Sioni kama utaratibu wa sasa wa kuonyesha aliyeua jambazi ni sahihi.

Aliyeua umeshamzawadia yeye hataki sifa kuonyeshwa kwenye magazeti kwani kunamletea hali hatarishi kwa usalama wake na familia yake.

LENGAI OLDOINYO
lengai2000@yahoo.co.uk

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.