MTANGAZAJI

MAENEO HATARI KWA USALAMA WA RAIA JIJINI DAR ES SALAAM

Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:
Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden nihatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi yalaptop na mapochi makwapani mwao.Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kishaabiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.

Mbagala:
Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwakuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu. Kundi hili hupora fedha,simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwavipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.

Giraffe Hotel:
Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuachamali za thamani ndani ya magari yao.Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunjavioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windowsna kuchukua kila wanachoweza.Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at ownersrisk.

Posta ya zamani na mpya:
Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogeshamagari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili. Watumia daladala waPosta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoniwakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu.Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaachandani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo yamaegesho.

Bonde la Jangwani, Salenda Bridge na Bonde la Kigogo:
Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanyahuo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatarizaidi. Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringihadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama.

Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuachaukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.

Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:
Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi nakupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi. Maeneo haya yametuliasana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakinihayana usalama wowote na ni hatari kabisa.Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili nanusu giza likiwa linaingi, maana utakumbwa na dhahama.

Daraja la Mlalakuwa, karibu na makao makuu JKT:
Hapa watu wamesema weeeee wamechoka. Yaani watu wanavyoporwa kila sikukijua kikizama inaanza kuaminika kwamba wapiga loba ni askari wa hapoJKT ama wanashirikiana na hao vibaka. Wakazi wanajiuliza iweje sehemu nyeti kama hiyo pawe na vibaka? Wanatokea wapi?TUTAFIKA kweli?Afande Kova upooooooooo????

NB: Sehemu ambazo hazijatajwa, ikiwa hata mikoani na visiwani,leteni habari
Michuzi Jr-2
-jamiothman@gmail.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.