MTANGAZAJI

UHARIFU KWA MTANDAO UNAOWEZA KUTOKEA MWAKA 2010

Mwaka 2010 ndio uko mwanzoni kabisa pamoja na ni vizuri tuangaliamatisho ya uhalifu unaoweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa mwakahuu ili wengi wetu waweze kuwa makini zaidi .

Si unajua kwamba mwaka huu kuna Michuano ya kombe la dunia nchiniAfrika ya kusini , wahalifu kadhaa wameanza na wengine wameshafanyamajaribio kadhaa ya kuuza tiketi feki kwa njia ya mtandao aukumdanganya mtembeleaji wa mtandao aingie kwenye tovuti ambazo nibandia kwa kujifanya zina mahusiano na kombe hilo la dunia ni mambokama hayo .

Je hili la kusajili namba za simu ? kusajili namba ya simuinakuwezesha wewe kuwa karibu zaidi na kampuni za matangazo kwahiyoutegemee kuletewa matangazo mengi sana kwenye simu yako ya mkono naaina nyingine ya uhalifu kwenye simu hiyo hiyo ya kiganja .

Pia kuna suala la kuangalia sana jinsi tunavyotembelea mitandao yajamii kama facebook au hi5 kuna wahalifu wanajificha kwenye mitandaohiyo kwa majina bandia au kuweka taarifa ambazo sio sahihi kwa ajiliya kuvutia watu ambao wanaweza kuangukia kwenye mikono ya wahalifu haomwishowe kutendewa vitendo viovu .

Ni wakati kwa kampuni mbalimbali zinazoruhusu wafanyakazi waokutembelea au kuweka taarifa zao kwenye mitandao hii kuwa na sheriamaalumu zinazohusu mitandao jamii kuweza kutetea maslahi ya kampunihizo kwenye mitandao ambayo inahusu jamii kama facebook bila kusahaukingine kwamba taarifa unazoweka kwenye mitandao hii au picha zakozinaweza kutumika dhidi yako wakati wowote bila ya wewe kutegemeakwahiyo ni vitu vya kuangalia sana .

Kwa wale wapenzi wa kutafuta vitu kwa njia ya mtandao kwenye searchengines nao wawe makini sana ni kweli kwamba kuna baadhi ya programuzinazoweza kutambua tovuti na linki mbaya lakini hili sio kwa asilimia100 na kwa sasa unaweza kutegeka na majibu unayoyapata kwenye tovutihizo ambazo ukitembelea unaweza kudownload program za kuharibu kompyuta yako na vitu vingine .

Kwa kipindi cha mwaka jana tumeona jinsi uhalifu ulivyofanyika kwenyemashine nyingi za ATM kwa habari nilizosoma kwenye vyombo kadhaa vyahabari zinasema kwamba Mashine nyingi za ATM zimekuwa na matatizo yahapa na pale ila sijasikia matukio mengine zaidi ya kuibiwa pesa kwanjia hii lakini kuna la kujifunza hapa kwanini Mashine nyingi zinapatamatatizo mara kwa mara ?

Uharibifu wa kitu kama Mashine hizi unaweza kumaanisha uthaifu wamashine hizo kwahiyo udhaifu huu unaweza kutumika na wahalifu kwaajili ya kufanya mashambulizi makubwa zaidi kwenye mashine hizi na kwanjia ya mtandao huko mbeleni kwahiyo watu wawe makini sana .

Na mwisho ni kuhusu mwendo wa huduma za mtandao kwa sasa ulivyokuwa wakasi kuliko ulivyo huko nyuma , hii inaweza kuvutia wahalifu kwanjia moja au nyingi na ukizingatia hatuna sheria za masuala yamitandao inawezekana kabisa nchi yetu ikageuka shamba la mashambuliziya kimtandao kama hali ikiachiwa kuendelea kama ilivyosasa .

Tusisahau mwendo huu wa mitandao umesababisha watu wengi pia wawezekuchukuwa vitu haswa program nyingi kwa njia ya mtandao ambapomitandao mengine inatoa program hizi kwa njia ambazo sio halali hiziprogramu zinaweza kuwa na virus ndani au aina nyingine ya programu zakiuhalifu.

Ni vizuri kampuni na mashirika ya umma kuwa na sera zao zinazohusumatumizi ya mitandao na vifaa kama komputa na kadhalika ili kuwezakukabiliana na hali hii kwa sababu kampuni nyingi sana zimekubalikuuziwa programu hizi pasipo kujua au wafanyakazi wa kampuni hiziwameuziwa programu hizi pasipo wao wenyewe kujua na matokeo yake nikufanya uhalibifu ambao kungekuwa na taratibu nzuri ungewezakuzuilika .

Haya ni maoni yangu tu hayahusiani na kampuni yoyote au kikundichochote cha watu .
Yona F Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.