MTANGAZAJI

UTATUZI WA ONGEZEKO LA MAGARI NCHINI TANZANIA

(kaka Maduhu nakuomba uwawekee wananchi wenzangu waone; huu ni mtazamo wangu tu!)

Habari ndugu wananchi wenzangu, napenda kupendekeza mambo machache yafuatayo kwani tumeshuhudia kuna ongezeko kubwa sana la idadi ya magari hasa katika miji mikubwa nchini kama vile Dar, Arusha na Mwanza. Ongezeko la idadi ya utumiwaji wa magari linachangia kwa kiasi kikubwa sana katika ongezeko la hewa chafu ambazo huleta madhara kwa binadamu na viumbe wengine kwa ujumla.

Yafuatayo ni mapendekezo yangu:-

(1) Tukumbuke kwamba ongezeko la magari nchini/mijini linachangia kwa kiasi kikubwa sana katika ongezeko la hewa chafu kama carbondioxide (CO2), methene (CH4) etc. Gesi hizi zinachangia sana katika ongezeko la joto duniani ambalo linachangia katika kuharibu mabadiriko ya hali ya hewa kama mvua nyingi (mafuriko), joto kali na hata matatizo makubwa kama tsunami ya mwaka 2007. hivyo serikali haina budi kuwatoza watumiaji wa magari 'kodi' ambayo ni ya 'uchafuzi wa mazingira' i.e carbon tax, methane tax, etc.

(2) suala la kutoza ada kubwa kwa watu wanaotaka kuingia katikati ya jiji na magari yao ni zuri. Lakini watu wanye pesa zao watatoa tu!! Je? vipi kwa mwananchi wa hali ya kawaida atamudu? jibu nu HAPANA. Natoa ushauri kwa manispaa kwamba wakati sasa umefika wa kupanua barabara si kwa kuongeza ukubwa wa barabara!! bali wa kuongeza 'root' nyingi! mradi huu unahitaji mtaji kwani barabara inabidi zihandisiwe juu na chini kiasi kwamba zirahisishe usafirishaji. Pia serikali ingeanzisha mradi wa city train (metro) za juu na chini ya ardhi kuzunguka jiji/miji mikubwa kama Dar, Arusha, Mwanza n.k

(3) Serikali ingehimiza utumiwaji wa benzene (C6H6), CNG (compressed natural gas) na LPG(liquefied petroleum gas)kuwa/kama chanzo cha nishati kwa watumiaji magari. Tunajua magari mengi yanatengenezwa ili yatumie gasoline (petroli) au diesel; hivyo serikali ifanye mpango wa kununua teknologia kutoka katika nchi zilizo endelea kuhusu uundwaji wa vifaa ambavyo vitafungwa kwenye magari yatumiyao petroli au diesel ili yatumie nishati mbadala kama CNG, LPG, Benzene kwani hazina mkusanyiko mkubwa wa hewa chafu!

(4) Ifahamike kwamba gharama za mwanzo za vifaa hivyo ni ghali kwa mwananchi wa kawaida!! hivyo serikali haina budi ku 'subsidy' vifaa hivyo ili vipatikane kwa mwananchi wa kawaida. Hii inaweza ikatumiwa kama sera mbadala ili kulinda mazingira yetu. Angalia nchi ambazo zimeendelea; serikali zao zimeweza kufanikisha suala hili kwa zaidi ya asilimia 75.

(5) serikali haina budi kuwaelimisha wananchi wapendao kununua magari kwamba wanunue magari ambayo ni energy efficient. Hii itasaidia kupunguza idadi ya nishati ambayo hutumika kuendeshea magari hayo katika muda fulani. kwa mfano gari ambalo linatumia lita 1 kusafiri kilomita 20-22 ni bora kuliko gari ambalo linatumia lita 1 kusafiri kilomita 17. hii itapunguza sana hewa chafu kutoka katika magari.

(6) serikali haina budi kuanzisha mradi wa mabasi ya jiji ambayo yatasafirisha wananchi kwa gharama nafuu hivyo kuwafanya watu wengi kutumia mabasi ya jumuiya na kupunguza idadi ya magari mijini ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa katika kupunguza ongezeko la hewa chafu jijini na nchini kwa ujumla.

Mdau Felix Mwema aliyeko Thailand

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.