MAJI YANAPOKUWA BIDHAA ADIMU
Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Manispaa ya Morogoro eneo la Area Six wakiwa na ndoo zenye maji baada ya eneo hilo kukumbwa na uhaba wa Maji hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kutafuta maaji kwa ajili ya matumizi ya shule.
Hivi karibuni blog hii ilizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bweni ya Morogoro sekondari ambao pia wamekuwa wakikumbana na adha hii kwa muda mrefu baada ya huduma hiyo kukatwa kwa kile kinachodaiwa kuwa wanadaiwa bili ya maji!!!!
Je ni kosa la wanafunzi ama mamlaka zinazohusika? Mimi ninavyofahamu mwanafunzi wa bweni anapaswa apate huduma zinazomhusu ili asome na si jukumu la mwanafunzi hasa wa kike kwenda kutafuta maji ya kutumia kwa eneo lililonje na sehemu hiyo ya Bweni.Lakini utashangaa kila siku asubuhi nakutana na wanafunzi wa Morogoro sekondari wakienda kuchota maji nje ya eneo lao la shule mabya zaidi ni saa za masomo.
Kilichonishangaza ni kwamba huko wanakoenda kuchota wanapewa huduma hiyo bure lakini katika eneo la shule yao maji yamekwatwa basi kama ndo hivyo pengine serikali iwaaombe wazazi na walezi wao wawape pesa kwa ajili ya kulipia bili za maji!!!!!
Post a Comment