MTANGAZAJI

BREAKING NEWS

Habari zilizoifikia blog hii sasa hivi zinaeleza kuwa Mfanyakazi wa ndani mwenye umri kati ya miaka 15 na 17 amebakwa na akatwakatwa mapanga na mwili wake kuwekwa ndani ya kiroba, ni maeneo ya kilakala,hapa Morogoro asubuhi ya leo

Polisi wameshauchukua mwili wa huyo binti ambaye inasemekana ameuawa kikatili na mtu aliyeombwa kumsaidia Mama Cham ambaye ndiye mwenye nyumba kukata michongoma nyumbani kwa mama huyo,Mama Cham ni mfanyabiashara hapa Morogoro.Baada ya kufanya kitendo hicho mhusika ametoweka na hajulikani alipo

Chanzo cha habari kilichokuwa kituo kikuu cha Polisi Morogoro kinaeleza kuwa Mama Cham wakati anataka kupunguza michongoma yake alimuomba kijana mwingine ambaye anaishi nyumba ya jirani ili amtafutie mtu wa kumpunguzia michongoma na ndipo huyo kijana akamtafuta kijana mwingine ambaye inasemekana walishirikiana kufanya kitendo hicho kwani hata huyo kijana wa jirani naye hajulikani alipo

Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.